Emeresiana Athanas
Ummy Mwalimu |
SERIKALI imedhamiria kujenga vituo 100
vya kutoa huduma ya dharura kwa wanawake wenye matatizo ya uzazi vijijini.
Hayo yalisemwa Dar es Salaam juzi na Mkurugenzi
wa Mafunzo,Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk Otilia
Ogwelle wakati wa ufunguzi wa kongamano la tatu la afya nchini.
Dk Otilia alisema hiyo ni moja ya hatua
za kupunguza vifo vya wanawake vinavyotokana na uzazi ambapo vituo hivyo
vitakuwa vikitoa huduma za upasuaji bila kwenda hospitali za mkoa au wilaya.
Alisema lengo la Serikali ni kusogeza
upatikanaji huduma za afya kwa wananchi kwa kushirikiana na sekta binafsi
ambapo imedhamiria kufikisha asilimia 74 ya upatikanaji wa zahanati, vituo vya
afya na wataalamu wa afya katika maeneo mbalimbali.
Rais wa Kongamano hilo, Dk Omary Chilo
alisema upatikanaji wa huduma za afya nchini bado ni finyu, na kuweka wazi kuwa
kupitia mkutano huo uliokutanisha wadau utatoa fursa ya utoaji mapendekezo ya
namna ya kutatua tatizo hilo.
Alisema mkutano huo utajadili changamoto
kwenye sekta ya afya likiwamo suala la upatikanaji dawa na kuona namna ambavyo
viwanda hivyo vitaongezwa.
0 comments:
Post a Comment