Mlinzi wa Kanisa adaiwa kuiba gari


Jemah Makamba

MLINZI wa Kanisa la Free Pentekoste Tanzania, Juma Msumari (62), amefikishwa kwenye Mahakama ya Wilaya ya Ilala, kwa tuhuma za wizi wa gari aina ya Toyota Litence lenye thamani ya Sh milioni 18 mali ya kampuni ya Recycler.

Akisoma mashitaka jana, mbele ya Hakimu Mkazi Adelf Sachore, Mwendesha Mashitaka wa Polisi, Munde Kalombola alidai mshitakiwa alitenda kosa hilo kinyume na kifungu cha sheria cha 258 na 265 sura ya 16 kilichofanyiwa marekebisho mwaka 2002.

Alidai kuwa Agosti 20 maeneo ya Buguruni Madenge, akiwa mlinzi, aliiba gari hilo huku akijua ni kosa.  

Mshitakiwa alikana mashitaka na Hakimu Sachore kusema dhamana yake iko wazi kama atakidhi masharti.  

Kwa mujibu wa Hakimu huyo, Msumari alitakiwa kuwa na wadhamini wawili wa kuaminika na wanaofanya kazi katika taasisi zinazofahamika watakaoweka dhamana ya Sh milioni 9 kila mmoja.

Mshitakiwa alishindwa kukidhi masharti ya dhamana na kurudishwa rumande na kesi yake itatajwa Novemba 22.  
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Laptop City

Tangazo