Mshamu Ngojwike
KWA sasa Ligi Kuu Tanzania Bara
ilipofikia ni zaidi ya fainali, hilo halina ubishi kutokana na miamba ya soka nchini,
Simba na Yanga kuhitaji pointi kila mechi.
Kwa lugha nyepesi unaweza kusema utamu
sasa umekolea kwani hakuna timu inayohitaji kupoteza pointi kijinga na kumpa
mwenzake faida.
Utamu huu unakolezwa kutokana na vita
iliyopo kwa miamba miwili ya Ligi Kuu Tanzania Bara, Simba na Yanga ambao
wanawania kumaliza mzunguko huu zikiwa kileleni mwa msimamo wa ligi hiyo.
Simba wao wana akili ya kutopoteza
mchezo wowote ili kuepuka kukutwa na wapinzani wa Yanga ambayo inashika nafasi
ya pili ikiwa na alama 27, nyuma ya alama tano na vinara wa ligi, Wekundu wa
Msimbazi.
Achana na kukutwa na Yanga, lakini Simba
inahitaji kulinda heshima yake ya kutopoteza mchezo msimu huu, ambapo katika
michezi 12 waliyocheza hakuna waliyofungwa.
Yanga inahitaji kushinda mechi
zilizosali, ili nao wasiruhusu alama nyingi kupitwa na Simba inayoongoza
msimamo huo wa Ligi kuu Tanzania Bara.
Yanga inaamini endapo ikipoteza mchezo ama
kutoka sare na timu yoyote ile ni kuipa kiburi Simba na kuzidi kutanua kileleni
mwa msimamo huo ambao wameachwa kwa idadi kubwa ya pointi.
Katika Makala haya, nakuletea kile kilitokea
kwenye michezo iliyopita ya Ligi Kuu Tanzania Bara kwa timu zote.
Simba
inaukuta wa chuma
Simba msimu huu imeonekana kuwa makini
kuanzia safu ya ulinzi kuwa imara ambao wameruhusu mabao machache kuliko timu
nyingine yoyote ya Ligi Kuu Tanzania Bara.
Hadi sasa Simba imefungwa mabao matatu
tu, katika michezo 12 iliyocheza wakati ikifunga mabao 24 na kuongoza msimamo
wa ligi hiyo ikiwa na alama 32.
Hii inatokana na maelewano ya mabeki wao
wa kati, Method Mwanjale ambaye anaungana na Juuko Murshid na Novaty Lufunga
aliyekuwa katika kiwango bora msimu huu.
Fowadi
ya Yanga tishio
Hakuna safu ya ushambuliaji iliyotishio
msimu huu kama ya Yanga kwa timu zote zinazoshiriki Ligi Kuu Tanzania Bara.
Yanga imefunga mabao 27 katika michezo
12 iliyocheza, lakini ikiruhusu kufungwa mabao matano tu, hivyo kuwa na wastani
mzuri wa kupachika mabao ukiacha timu zote za Ligi Kuu Tanzania Bara.
Washambuliaji wake wanne, Amis Tambwe,
Donald Ngoma, Simon Msuva na Obrey Chirwa wamefunga mabao 21 msimu huu
ikiwaacha washambuliaji kibao katika timu nyingine.
Majimaji
kinara wa kuachia
Ukiacha kuburuza mkia katika msimamo wa
Ligi Kuu Tanzania Bara, lakini Majimaji ndiyo klabu iliyoruhusu kufungwa idadi
kubwa ya mabao msimu huu.
Katika michezo 13 iliyocheza Majimaji
msimu huu, imeruhusu mabao 23, ikifunga mabao 10 tu licha ya kufanya mabadiliko
kwenye benchi la ufundi.
0 comments:
Post a Comment