Mery Kitosio, Arusha
Mbunge wa Arusha, Godbless Lema |
MBUNGE
wa Arusha Mjini, Goodbless Lema (Chadema), aliyepewa jina Rais mteule wa
Marekani, Donald Trump, amerudishwa rumande baada ya mawakili wa Serikali kumkatia
rufaa ya kupinga hukumu ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha, iliyomwachia huru
kwa dhamana jana.
Hatua
hiyo imekuja baada ya Hakimu Desideri Kamugisha wa mahakama hiyo kutoa uamuzi
mdogo wa kumuachia kwa dhamana mshitakiwa huyo, baada ya kuridhika na hoja
zilizotolewa na mawakili wa upande wa utetezi.
Katika
hoz hizo, mawakili hao wa utetezi, wakiongozwa na Wakili Sheik Mfinanga, waliitaka
mahakama hiyo impatie dhamana Lema kwa madi kuwa kosa linalomkabili linastahilii
kupatiwa dhamana.
Hata
hivyo baada ya hukumu hiyo ndogo, mawakili wa Serikali wakiongozwa na Paulo
Kadushi na Materrus Marando, waliwasilisha ombi la mdomo la kukusudia kukata
rufaa kupinga hukumu ya mahakama hiyo.
Kuwasilishwa
kwa kusudio hilo la mawakili wa Serikali, kulisababisha Hakimu Kamugisha
kuahirisha kwa muda wa dakika kumi usikilizwaji wa shauri hilo na baadae
aliporejea, alisema mahakama hiyo haiwezi kuendelea na shauri hilo.
Hakimu Kamugisha
alifafanua kuwa tayari upande wa Serikali wamefungua kesi ya kukata rufaa mahakama
ya juu, ikidai kuwa mahakama yake haina uwezo wa kuendelea na shauri hilo, hadi
Mahakama ya Rufaa itakapotoa uamuzi.
Kutokana
na hatua hiyo, Mbunge Lema alirudishwa rumande kusubiri kesi hiyo ya rufaa
ipangiwe jaji wa kuisikiliza.
Wakati
huo huo Lema pamoja na mkewe Neema, wanatarajiwa kupanda kizimbani kesho kutwa
katika kesi ya uchochezi inayowakabili dhidi ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha.
Wafuasi
wa Lema waliokwenda kusikiliza kesi hiyo, walimshangilia kwa nguvu mbunge huyo
wakati akipandishwa kwenye basi la Magereza huku wakimuita kwa jina la Donald Trump.
0 comments:
Post a Comment