Neema Sawaka, Kahama
Fadhili Nkurlu |
Akizungumza
wakati akikabidhi vifaa hivyo jana Meneja wa Mgodi wa
Acacia Buzwagi, Asa Mwaipopo alisema kampuni hiyo imetoa msaada
huo baada ya kutembelea hospitali hiyo na
kushuhudia wagonjwa wakibebwa mgongoni badala ya viti vya magurudumu au machela.
Mwaipopo alisema waliguswa
na hali hiyo na kutoa vifaa tiba ili kupunguza tatizo la vifaa na kuboresha
huduma na kusaidia kuokoa maisha
ya watu.
Alitaja vifaa
tiba vilivyotolewa kuwa ni mashine tatu za oksijeni, viti vya
magurudumu vitano, machela, mashine ya ufuatiliaji mapigo ya moyo na mashine ya
kusafishia vifaa vya upasuaji.
Akipokea
msaada huo, Mkanga Mkuu wa Halmashauri ya Wilaya, Bruno
Minja alishukru wawekezaji hao na kuongeza
kuwa hospitali inakabiliwa na msongamano mkubwa wa wagonjwa kutoka halmashauri
za Ushetu, Msalala, Urambo, Tabora, Ulyanhulu na Kaliua.
Alisema vifaatiba
hivyo ni msaada mkubwa na muhimu sana kwao ambapo kwa siku
hospitali inahudumia wagonjwa 600.
Mkurugenzi wa
Halmashauri ya Mji, Underson Msumba aliushukuru uongozi
wa Buzwagi akisema wamekuwa wadau wakubwa wa maendeleo ambapo
wamesaidia kuboresha huduma za jamii katika sekta za afya, maji
na elimu.
Mkuu wa Wilaya, Fadhil
Nkurlu aliwataka madaktari na wauguzi wa hospitali hiyo
kutunza vifaa hivyo na kuhakikisha vinatumika kwa
malengo yaliyokusudiwa.
0 comments:
Post a Comment