Emeresiana Athanas
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira,
Januari Makamba amesema watu wanaopinga Muungano huku wakimsifu Baba wa Taifa,
Mwalimu Julius Nyerere ni wanafiki.
Akizungumza Dar es Salaaam jana, Makamba alisema hata maisha
aliyoishi Mwalimu Nyerere na kuyapigania wakati wa uhai wake, ni watu wachache
wanaoishi maisha hayo sasa, badala yake wengine wameamua kumtumia vibaya kwa
kushinikiza mambo wanayotaka au kupinga wasiyotaka.
“Huo tunaita unafiki, kwani huwezi kusema Muungano haufai, lakini
Mwalimu anafaa, itakumbukwa kuwa Mwalimu alitoa machozi mwaka 1993, wakati
kundi la wabunge walioitwa G55, walipoleta hoja ambazo zingesababisha kuvunjika
kwa Muungano, alitoka kijijini na kuja kuhakikisha Muungano unapona na kudumu,”
alisema Januari.
Alisema kutokana na hatua hiyo, Muungano ni moja ya mambo
yanayotakiwa kuenziwa pamoja na maadili ya uongozi, kwani ni mambo aliyokuwa
akiyasimamia.
Kwa mujibu wa Makamba, miongoni mwa mambo aliyosimamia Mwalimu
Nyerere mbali na Muungano ni pamoja na kurudisha nidhamu kazini, kupinga rushwa
na ufisadi ambayo kwa sasa yanasimamiwa na Rais John Magufuli.
“Yapo mambo ambayo Rais anayafanya kwa sasa kuleta nidhamu, kupinga
rushwa na ufisadi ni mambo ambayo yanaturudisha kwenye misingi yake (Nyerere).
“Maadili ya umma ni niongoni mwa mambo tunayotakiwa kuyaenzi kwani
ukishakuwa kiongozi wa umma, kuna baadhi ya mambo ambayo unatakiwa uyakose na
bahati mbaya kwa sasa viongozi wa umma wanataka kupata vyote, heshima na
utajiri,” alisema.
Alisema ipo kazi ya kuendelea kumuenzi Mwalimu, kwani kwa miaka 17
sasa tangu alivyofariki dunia bado kuna changamoto nyingi
0 comments:
Post a Comment