Mwandishi Wetu
CHAMA cha ACT Wazalendo kimetaka mchakato wa kuandika Katiba Mpya
uanze kwa kufanya Marekebisho ya Sheria ya Kura ya Maoni, kikimshauri Rais John
Magufulikuunda timu ya wataalamu, kupitia Rasimu ya Katiba ya Jaji Joseph
Warioba, kuitisha mkutano wa kikatiba ili kupitisha Katiba Pendekezwa hadi
kufikia hatua ya Kura za Maoni
Kwa mujibu wa maazimio yaliyofikiwa na mkutano wa kwanza wa kisera
wa chama hicho tangu kumalizika kwa Uchaguzi Mkuu, ACT imesema kuna umuhimu wa marekebisho
kwa sheria hizo na ile ya Mchakato wa Katiba kwa muastakabali wa Taifa.
Chama hicho pia kimetaka kujalidiwa kwa Azimio la Arusha katika miaka
25 ya kutekelezwa kwake na madhara yake tangu lilipozikwa visiwani Zanzibar
mwaka 1992.
“Chama kimeazimia mchakato wa kuandika Katiba Mpya uanze kwa
kufanya marekebisho ya Sheria ya Kura ya Maoni na Sheria ya Mchakato wa
Katiba,” ilisomeka sehemu ya maazimio hayo.
Kwa mujibu wa maazimio hayo iwapo Serikali itaamua kwenda na Katiba
Pendekezwa iliyopo sasa, ACT itaipinga kwa kufanya kampeni za HAPANA kwenye
kura ya maoni.
Kwa mujibu wa ACT, wakati mchakato wa Katiba ukiwa umesimama Baraza
la Wawakilishi la Zanzibar limepitisha Sheria ya Kutafuta Mafuta na Gesi
kinyume na matakwa ya Katiba ya Muungano inayoeleza mafuta na gesi ni masuala
ya Muungano.
Mkutano Mkuu wa Kidemokrasia ACT pia umeshauri mbunge wake, Zitto
Kabwe ambaye pia ni kiongozi wa chama hicho kuwasilisha muswada binafsi wa
Mabadiliko ya Katiba ya Muungano yanayolenga kuondoa mafuta na gesi kwenye
mambo ya Muungano.
Kwa mujibu wa maazimio hayo ya ACT, kufanya hivyo kutaiwezesha
Zanzibar kuendelea na utafutaji na uchimbaji wamafuta na gesi asilia bila
vikwazo vya kiufundi kwa ajili ya kikatiba.
0 comments:
Post a Comment