Dalila Sharif
IGP Mangu |
WAKAZI
wa Mtaa wa Mkondogwa, kata ya Chamanzi, Temeke wameliomba Jeshi la Polisi na
Polisi Jamii kudhibiti ujambazi kwenye kituo cha mabasi cha Lulu mtaani humo.
Wakizungumza
na mwandishi wa habari hizi kwa nyakati tofauti jana, wakazi hao walisema
matukio mengi ya ujambazi hutendeka eneo la kituo hicho na kuhatarisha maisha
ya watu.
Mwenyekiti
wa Mtaa huo, Nassoro Lukindo alithibitisha kuwepo kwa hali hiyo na kueleza
kwamba matukio hayo yanafanyika kwenye mtaa wake kwa kutumia silaha za moto
wakivamia maduka na kupora pesa.
“Vema
walinzi shirikishi kujitokeza na kuendelea kuimarika katika mapambano ya
kudhibiti uvamizi wa kutumia silaha na wezi na Jeshil la Polisi kutusaidia ili
kuondoa uhalifu huo,” alisema Lukindo.
Mmoja wa
wakazi wa eneo hilo, Hamidu Hamdu alisema hali si shwari kutokana na kukithiri
uvamizi na kuwasababishia woga wakazi wa
eneo hilo na abiria wanaotumia kituo wakihofia kuporwa na kuhatarisha maisha
yao.
“Siku
mbili zilizopita, kulitokea uvamizi wa uporaji wa kutumia silaha za moto na
kuvamia baadhi ya maduka katika eneo hili, hali ambayo matukio haya hujirudia
huku tukihofia usalama wetu,” alisema Hamdu.
Mary
Johson wa mtaa huo alisema ni vema Jeshi la Polisi likaongeza ulinzi ili kudhibiti
matukio hayo yanayotokea ili kuzinusuru mali na usalama wa maisha ya wakazi na
wageni wa eneo hilo.
“Licha
ya kuwa na Polisi Jamii haiwezi kusaidia pekee katika kudhibiti watu wanaotumia
silaha ni vema kuwa na umoja katika kutoa taarifa mapema ili kudhibiti matukio
hayo,” alisema Mary.
0 comments:
Post a Comment