Grace Gurisha
MKURUGENZI wa Kampuni ya Afrilulu, Anthony Gulfer (47),
ambaye anatuhumiwa kukutwa na kobe zaidi ya 100 wenye thamani ya Sh milioni 18,
leo anatarajiwa kupandishwa kizimbani kwa mara ya pili katika Mahakama ya
Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam kuangalia kama upelelezi umekamilika au la.
Gulfer ambaye ni raia wa Australia anatarajiwa kufikishwa
mahakamani hapo mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi, Thomas Simba wakati kesi yake
inapokuja kwa kutajwa na kuangalia kama upelelezi umekamilika au la.
Wakili wa Serikali, Baltrida Mushi ataieleza Mahakama
hatua ya upelelezi ilikofikia, kwa sababu awali aliomba siku nyingine ya
kutajwa kwa kesi hiyo ili wakakamilishe upelelezi huo.
Ilidaiwa kuwa Machi 10, maeneo ya Kilomoni Kunduchi Dar
es Salaam, Gulfer alikutwa na nyara za Serikali, wakiwamo kobe wanne aina ya
Tinged, pia 108 aina ya Leopard na wengine wanne aina ya Aldabra.
Inadaiwa kuwa kobe wote hao wana thamani ya dola za
Marekani 8,190 sawa na Sh milioni 18,312,840. Mushi alieleza kuwa upelelezi wa
kesi hiyo haujakamilika na kuomba siku nyingine ili kutajwa.
Hakimu Mkeha alisema kutokana na Mahakama hiyo kutokuwa
na mamlaka kuhusu dhamana, mshitakiwa anaweza kwenda kuomba Mahakama Kuu.
0 comments:
Post a Comment