Mwandishi Wetu
Esther Bulaya |
MBUNGE wa Bunda Mjini, Esther Bulaya
(Chadema) ameitaka Serikali kueleza ilivyojipanga kukabiliana na ujambazi mkoani
Mara licha ya kujitokeza katika maeneo mengi nchini.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,
Hamad Masauni alisema Serikali inatambua kuwa hivi karibuni kumeibuka wimbi la
matukio ya kihalifu hivyo si kwa mkoa huo tu, bali kila eneo.
Alikuwa akijibu swali la Bulaya bungeni
jana ambapo alisema katika kukabiliana na hayo, Jeshi la Polisi nchini
limeendelea kubuni mikakati kadhaa na linafanya uchambuzi wa mwenendo wa
matukio hayo na kuwapa mbinu askari ya kuja na mikakati.
Alisema hatua nyingine ni kutabiri
matukio ya uhalifu kwa kutumia takwimu na mabadiliko ili kutambua wahusika,
wanakoishi na namna ya kukabiliana nao.
Aliongeza kuwa wamejipanga kutambua
maeneo ambayo yamekuwa yakitumika kama vituo vya uhalifu na kufanya msako kwa
doria, kuimarisha ulinzi nchini na kuchukua hatua kali kwa wahusika
wanapobainika.
Katika swali la nyongeza Bulaya alisema
kufanya doria ni jambo zuri lakini haliwezi kufanyika bila magari mazuri na ya kutosha
akihoji mkakati wa Serikali kutoa gari jipya ili kusaidia doria.
Masauni alisema alilichukua swali hilo kama
changamoto na kwamba magari yakipatikana mkoa huo utakuwa wa kwanza kupewa ili
kuwezesha askari kwenye doria.
Aidha, alisema kuwa eneo la Tunduma mkoani
Mbeya, nalo ni changamoto kwa uhalifu, kwa kuwa liko mpakani hivyo
watahakikisha nalo linachukuliwa hatua mapema.
0 comments:
Post a Comment