Mary Mtuka
SHIRIKA la Maendeleo la Kimataifa la
Japani (JICA) limetoa msaada wenye thamani Sh bilioni 36 katika kuendeleza
sekta ya maji mkoani Tabora.
Taarifa iliyotolewa jana na Mwakilishi
Mkuu wa JICA nchini, Toshio Nagase amesema msaada huo utaongeza wigo wa
usambazaji maji safi na salama vijijini mkoani humo.
"Ni mara ya kwanza nchini mradi
mmoja kufanikiwa kuchimba jumla ya visima virefu 115 katika eneo kame kama
Tabora ambao hali yake ya kihadrolojia si rafiki kupata maji safi na
salama," alisema.
Alisema mradi huo utanufaisha watu zaidi
ya 40,000 ambao watapata maji safi na salama kwenye vijiji kusudiwa ikiwa ni
ongezeko la asilimia 30 kutoka asilimia 9.9 ya mwaka 2009.
Nagase alisema Shirika hilo lilipokea
maombi ya kuchimba visima na kufanya utafiti wa awali kuanzia mwaka 2009 hadi
2011 ambapo uchimbaji rasmi ulikamilika mwaka jana.
Aidha, alisema mwanzoni mradi huo
ulipata changamoto kama za ugumu wa kupata vyanzo sahihi vya maji safi na
salama.
Alisema mradi huo ulihusisha ufungaji
pampu za mikono na ujenzi wa miradi minne ya kusambaza maji na ujenzi wa sehemu
za umma za kuchotea maji.
Mwakilishi huyo alisema mbali na ujenzi
wa miundombinu ya maji, mradi huu pia umesaidia mkoa na wilaya kuanzisha na
kusajili vyama vya kijamii (COWSOs) kwa ajili ya kusimamia uendeshaji na
matengenezo ya miundombinu ya maji iliyokamilika.
0 comments:
Post a Comment