Joyce Kasiki, Dodoma
Shukuru Kawambwa |
MBUNGE wa Bagamoyo, Dk Shukuru Kawambwa
(CCM), ameiomba Serikali kupeleka fedha kwenye Halmashauri ya Wilaya ya
Bagamoyo kujenga jingo la kitengo cha wagonjwa wa nje (OPD) la hospitali ya
wilaya hiyo.
Mbunge huyo alitoa kauli hiyo jana
alipouliza swali la nyongeza bungeni akihoji Serikali kama itakuwa tayari
kupeleka fedha kwa ajili hiyo akisema jingo hilo linahitaji kujengwa upya na si
kufanyiwa ukarabati.
Awali katika swali la msingi, Dk Kawambwa
alitaka kujua mpango wa Serikali kuboresha huduma za afya katika hospitali hiyo
kwa kuhakikisha upatikanaji wa miundombinu bora, vitendea kazi na kuiongeza
watumishi na dawa za kutosha.
"Kwa muda mrefu sasa huduma za afya
katika hopsitali ya wilaya ya Bagamoyo ni dhaifu sana kutoka na upungufu wa
miundombinu, vitendea kazi, uhaba wa watumishi na ukosefu wa dawa, Serikali ina
mpango gani wa kuboresha huduma za afya katika hospitali hiyo?" Alihoji Dk
Kawambwa
Akijibu, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya
Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Selemani Jafo alisema katika mwaka
wa fedha wa 2017/18, Serikali imetenga Sh 1,465,740,000 za kuboresha huduma za afya
katika hospitali hiyo ikiwa ni pamoja na kuboresha miundombinu na upatikanaji
dawa na vifaa tiba.
"Vile vile, zimetengwa Sh milioni
185 kwa mwaka wa fedha 2017/18 kutokana na ruzuku ya maendeleo kwa ajili ya
ujenzi na ukarabati wa miundombinu ya vituo vya kutolea huduma za afya, Sh
59,790,600 kutokana na mapato ya ndani kwa ajili ya upanuzi wa wodi ya wazazi, ukarabati
wa OPD, eneo la kuhudumia wagonjwa wa dharura na kumalizia ukarabati wa wodi ya
wanaume," alisema Jafo.
Aidha, alisema Serikali imetoa kibali
cha kuajiri madaktari na watumishi wengine wa afya huku Halmashauri hiyo pia
ikipewa kipaumbele.
0 comments:
Post a Comment