Rais John Magufuli |
RAIS John Magufuli, amemaliza ziara ya
siku tatu mkoani Kilimanjaro, ambapo pamoja na mambo mengine, alikuwa mgeni
rasmi katika maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani, Mei Mosi.
Katika maadhimisho hayo, Rais alitangaza
kuboresha mishahara ya wafanyakazi kulingana na madaraja, huku akiahidi
kupandisha mishahara mwakani.
Ziara ya Rais Magufuli ilianza Jumamosi
iliyopita akipokewa na wananchi wa mkoa huo waliomsindikiza kuanzia Boma
Ng’ombe hadi Moshi Mjini.
Akizungumza katika ziara hiyo, Rais
Magufuli alisema hajawahi kuona mapokezi makubwa ya kiwango hicho ambapo pia
aliwaambia amewasamehe na wao wamsamehe.
Pia Rais Magufuli alikutana na viongozi
wa dini mkoani humo na kuzungumza nao masuala ya maendeleo na kuwataka
wamwombee asiwe na kiburi.
Katika ziara hiyo, viongozi wa dini
walimpongeza kwa kuongoza nchi kwa amani huku wakimtaka kusimamia haki za
binadamu.
Katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa
Kilimanjaro (KIA), Rais Magufuli aliagwa na viongozi wa mkoa huo wakiongozwa na
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Said Meck Sadick.
0 comments:
Post a Comment