Utoro, mimba vyakatiza masomo wanafunzi 40


Jumbe Ismailly, Ikungi

WANAFUNZI 40 wa Sekondari ya Ikungi, mkoani Singida hawakumaliza masomo yao kutokana na sababu mbalimbali ukiwamo utoro na mimba katika kipindi cha kuanzia mwaka 2015 hadi sasa.

Mkuu wa Shule hiyo, Hango Mwanja alibainisha hayo kwenye taarifa ya shule katika mkutano wa wazazi ulioandaliwa kwa kujadili mbinu za kufanikisha ujenzi wa majengo ya maabara ya shule hiyo.

Mwanja alifafanua, kwamba wanafunzi 37 hawakumaliza masomo yao kutokana na utoro, huku wengine watatu kutokana na ujauzito katika kipindi cha kuanzia mwaka jana hadi sasa.

Hata hivyo, Mkuu wa Shule aliweka bayana kwamba jitihada za kuwatafuta waliotoroka na wazazi wao kutolea taarifa kwenye vyombo vya sheria, bado wanaendelea kutafutwa ili wakipatikana warudishwe shule kuendelea na masomo.

Mwenyekiti wa Bodi ya Shule, David Ntui alifafanua kuhusu sababu zinazochangia wanafunzi wa kike kupata mimba kuwa ni pamoja na hofu ya kutukanwa na wananchi na wazazi au walezi wa watoto hao kwa kuwawajibisha wanafunzi wanaobainika kujihusisha na vitendo vya ngono wangali shuleni.
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Laptop City

Tangazo