Mery Kitosio, Monduli
VIONGOZI wa kimila wametakiwa kutoa elimu kwa jamii
kuhusu madhara ya ukeketaji kwa watoto wa kike ili kupunguza vitendo hivyo.
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Shirika la Hinzi Makilini
Rumanyika wakati wa mjadala maalumu uliowakutanisha Malaigwanani wa Kata ya
Sepeko iliyopo Monduli.
Alisema wamekutana na viongozi wa kimila ili kujadili
tathimini ya masuala ya kampeni ya kupambana na ukeketaji wa watoto wa kike na
wanawake wa jamii ya wafugaji ya Kimasai kwani wao wamekuwa wakishirikiana nao
katika kumaliza tatizo hilo.
“Tumekutana na Malaigwanani wa rika mbalimbali ili
kuangalia mwenendo wa ukeketaji wa wanawake na watoto kwa jamii ya wafugaji wa
Kimasai, kwani tumebaini kuwa watoto chini ya miaka mitano wameanza kufanyiwa
vitendo hivyo wakati suala hilo kwa sasa linapigwa vita na tunahitaji
kulitokomeza kwa kushirikiana,” alisema Rumanyika.
0 comments:
Post a Comment