Salha Mohamed
SERIKALI imeokoa zaidi ya Sh. milioni 300 kwa ajili ya
kutibu watoto wenye matatizo ya usikivu hapa nchini.
Aidha, imesema itaanza kufanya uchunguzi kwa kutumia kifaa
maalumu mara watoto wanapozaliwa ili kubaini wenye matatizo hayo na kupunguza
idadi ya wanaokua wakiwa na matatizo ya usikivu nchini.
Hayo yalisemwa jana na mkurugenzi mtendaji wa hospitali
hiyo, Profesa Lawrence Museru katika uzinduzi wa huduma ya uwekaji wa programu
ya usikivu kwa watoto 45.
Profesa Maseru alisema kwamba upasuaji huo ulikuwa
ukifanyika nje ya nchi kwa Sh. bilioni 80 kwa kila mtoto.
Kwa mujibu wa Profesa Museru kumekuwa na ongezeko kubwa
la watoto wenye matatizo ya usikivu kila mwaka na hiyo ilitokana na tiba ya
upasuaji na uwekaji vifaa vya usikivu kutotolewa hapa nchini.
Alisema katika kipindi cha miaka mitatu ya awali serikali
ilitumia zaidi ya Sh. milioni 80 kwa mtoto mmoja kwa ajili ya kwenda nchini
India kwa ajili ya kuwekaew kifaa cha usikivu.
“Kwa sasa huduma hiyo inafanyika nchini baada ya nchi
kupata watalaamu wake wa ndani saba waliorudi kutoka masomoni nje ya nchi,”
alisema.
Alisema tiba hiyo kuanza kutolewa hapa nchini kumeokoa
zaidi ya Sh milioni 300 ambazo zingetumika kupeleka wagonjwa nje ya nchi.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,
Wazee na Watoto, Dk. Mpoki Ulisubisya alisema wazazi wanatakiwa kutambua
maendeleo ya ukuaji ya watoto wao ikiwamo afya.
Alisema tayari watoto 45 wameshafanyiwa ‘cochlea
implant’, ambapo alibainisha ‘ili kugundua watoto walio na tatizo hilo nchi
nzima, hadi Januari mwakani hospitali hiyo itaanza kuwafanyia watoto uchunguzi
tangu wanapozaliwa kwa kutumia vifaa maalumu.
Alisema idadi ya watoto wenye matatizo hayo wanaofikishwa
katika hospitali hiyo, ni ndogo ikilinganishwa na ambao wapo nyumbani au wazazi
hawajawagundua.
0 comments:
Post a Comment