Grace Gurisha
KATIBU Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam,
Theresa Mmbando ameieleza Mahakama jinzi alivyodhalilishwa kwa kushikwa matiti
na kukatiwa zipu ya sketi yake, katika kesi inayowakabili wabunge watatu wa
Chadema na madiwani wawili.
Wabunge hao ni wa Ubungo, Saed Kubenea, wa
Kawe, Halima Mdee na wa Ukonga, Mwita Waitara.
Madiwani ni wa kata ya Kimanga, Manase Mjema,
wa Saranga, Ephraim Kinyafu na kada wa chama hicho, Rafii Juma.
Mmbando alidai kuwa Februari 27 alipewa
jukumu la kusimamaia uchaguzi wa meya uliopaswa kufanyika kwenye ukumbi wa Karimjee
yeye akiwa Mwenyekiti wa Uchaguzi huo ambao ulitakiwa kufanyika saa 4 asubuhi,
lakini haukufanyika baada ya kutangazwa zuio la Mahakama.
Akiongozwa na Wakili wa Serikali,
Floretina Sumawe, Mmbando alidai mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Kisutu,
Dar es Salaam, Huruma Shahidi kuwa baada ya kutoa taarifa hiyo wajumbe wa CCM
walitoka nje, lakini wa vyama vingine walimvamia wakimtaka aendelee na uchaguzi
huo.
Alidai kuwa Mdee alivuta jalada lililokuwa
na mwongozo wa kikao hicho na kuondoka nalo na mama mmoja akampiga kwenzi
kichwani kwa kumshinikiza aendelee na mchakato huo, huku wengine wakimsukuma
kwa kumbamiza ukutani.
Shahidi huyo alidai kuwa Kubenea alimropokea
akimwita kibaraka wa CCM asiyeweza kuendesha Serikali kama mali yake, kwa hiyo
aendelee na kikao hicho huku Waitara akimsisitiza kuwa hawezi kuondoka hadi
kikao hicho kiishe.
Alidai kuwa Mjema alikuwa akituliza
wenzake wamwache ili waweke utaratibu kikao kifanyike, lakini wengine
walimshika kwa nguvu ili asiondoke hadi wakafikia hatua ya kumdhalilisha kwa
kumshika matiti bila idhini yake na huku
sketi ikivuka baada ya zipu kukatika, ambapo aliokolewa na polisi na kutolewa
nje.
Kesi hiyo itaendelea kusikilizwa Desemba
8. Akisoma maelezo hayo, Wakili wa Serikali, Flora Masawe alidai mbele ya
Hakimu Mkazi, Huruma Shaidi kuwa Februari 27, washitakiwa wakiwa Karimjee,
Ilala walimpiga na kumjeruhi Mmbando na kumsababishia majeraha mwilini.
0 comments:
Post a Comment