Warioba Igombe, Morogoro
Akithibitisha kuwepo kwa kunguni mmoja wa wazee hao, Ally Yusufu alisema wadudu hao wamekuwa wakiwanyima usingizi usiku na kutamani kupambazuke mapema.
Yusufu alisema kunguni ni wengi na usiku badala ya kulala usingizi hujikuta wakilia wakikumbuka maisha waliyoishi enzi za ujana wao tofauti na sasa.
“Mbali na vitanda tunavyolalia kuwa na kunguni, lakini pia ukutani na darini wamejaa na wamekuwa wakitunyima usingizi usiku,” alisema Yusufu.
Alisema hali hiyo huwafanya kuona uzee ni kitu kibaya katika maisha ya binadamu.
Kutokana na kilio hicho Yusufu aliiomba Serikali kuondoa tatizo hilo ili nao waishi kama binadamu wengine, kwani kuishi kwao kwenye kituo hicho hawakupenda, lakini iliwalazimu kufanya hivyo.
Rashid Omar ambaye ni Kaimu Msimamizi Mkuu wa Kituo hicho, alisema sumu ya kunguni ilishapulizwa katika kila chumba na kwamba wataendelea kufanya hivyo kuhakikisha kunguni wote wanakufa.
Aidha, alisema kituo hicho kinakabiliwa na changamoto ya kukosa vitendea kazi vya usafi ambapo alitaka wananchi kutoa ushirikiano katika utunzaji wa wazee hao kituoni hapo.
0 comments:
Post a Comment