Suleiman Msuya
ALIYEKUWA Mbunge wa Bunda, Stephen
Wasira ametaka Watanzania kuendelea kuishi kwa matumaini kwa kufanya kazi na kujiletea
maendeleo.
Aidha, amekanusha taarifa za kuhusishwa
na kugombea ubunge wa Bunge la Afrika Mashariki (EALA) na kwamba bado
anapambania ubunge wake wa Bunda Mjini.
Wasira alisema hayo jana alipozungumza
na JAMBOLEO akisema mwaka huu ni wa kufanya kazi ili kufuta machungu ya mwaka jana.
Alisema Watanzania hawapaswi kukata
tamaa ila kinachohitajika ni kufanya kazi kwa nguvu zote, ili kuchochea
maendeleo ya nchi na wao wenyewe.
"Niwatakie heri ya Mwaka Mpya, ila
tunapaswa kuishi kwa matumaini kuwa siku moja mambo yatakuwa mazuri,
kinachohitajika ni kuchapa kazi," alisema.
Mbunge na Waziri huyo wa zamani, alisema
hakuna sababu ya jamii kuangalia mtu fulani afanye jambo fulani ili kuleta
maendeleo na kwamba njia sahihi ni ushirikiano.
Kuhusu ubunge wa EALA alisema habari
hizo ni za uzushi na hazina ukweli wowote.
Alisema hajafikiria wala hana mpango wa
kugombea ubunge huo, kwani akili yake iko
Bunda Mjini kuliko na kesi ya kupinga matokeo.
Wasira alisema waliomtaja kuwa atagombea
EALA anawapongeza, lakini anapenda kuwahakikishia kuwa hatagombea.
Hivi karibuni gazeti ambalo linatoka kwa
wiki mara moja lilimtaja Wasira kuwa anatarajia kugombea ubunge EALA.
0 comments:
Post a Comment