Sijawa Omary, Mtwara
Rai hiyo ilitolewa jana na Kaimu Meneja wa Chama Kikuu cha Ushirika cha Masasi (MAMCU), Kelvin Rajabu wakati wa mkutano na waandishi wa habari mkoani hapa juu ya taarifa za mchakato wa zao hilo kwenye msimu huu wa 2016/17.
Alisema kutokana na uelewa huo mdogo wa viongozi hao imesababisha upotevu mkubwa wa baadhi ya fedha za wakulima wakati wa malipo kwa wakulima hao.
“Baadhi yao wamekuwa wakiongezwa fedha wakati wa kuwalipa fedha, wakulima wengine wana moyo na wamekuwa wakizairudisha lakini wasio na moyo wa kurudisha ‘wanaingia mitini’,” alisema Rajabu.
“Kwa hiyo, Serikali ni vema ikaliangalia hili na
kutusaidia kwani uovu unaanzia chini kwa hawa watendaji wetu wa ushirika na ndiyo wanaotuaangusha,” aliongeza.
Alisema hali hiyo inasababisha malalamiko kwa baadhi ya
wakulima kutolipwa stahiki zao kwa wakati.
0 comments:
Post a Comment