Wapima tezidume iliyokithiri


Joyce Anael, Moshi

IDADI kubwa ya wanaume wanaofika kwenye Hospitali ya Rufaa ya KCMC, mjini hapa kupima saratani ya tezidume, hugundulika kuathirika kwa kiwango kikubwa na ugonjwa huo.

Mkuu wa Idara ya Tiba ya Njia ya Mkojo ya KCMC, Dk Frank Bright alibainisha hayo juzi alipozungumza na mwandishi wa habari hizi ofisini mwake akisema wagonjwa wengi huwa wamefikia hatua mbaya ya saratani hiyo hivyo kukosa uwezekano wa kupona tena.

Alisema katika KCMC imekuwa ikipokea wagonjwa zaidi ya 100 katika kitengo cha mkojo kwa mwaka na kati yao, zaidi ya asilimia 60 hufika wakiwa wameathirika zaidi.

Aidha, alisema rika la watu wanaoathirika zaidi na ugonjwa huo, ni wanaume wenye umri wa kuanzia miaka 60 na kuendelea na kwamba wananchi wengi wamekuwa hawana mwamko wa kupima ugonjwa huo, kwa kuhofia namna ya upimaji na kuona ni ugonjwa wa aibu.

Alisema katika kuhakikisha ugonjwa huo hauendelei kukua kwa kasi, kuna haja ya elimu kutolewa kwa kina katika jamii, ili kutoa mwamko wa watukujitokeza kwa wingi kupima na kuona ni ugonjwa kama mengine.

“Wananchi wengi hawana ufahamu wala uelewa wa ugonjwa huu na wengine wakiusikia wanaona kama ni ugonjwa wa aibu, hili ni tatizo na kunahitajika nguvu zaidi katika utoaji elimu na kuhamasisha watu kujitokeza kupima ili wanaogundulika wapate matibabu kabla hali haijawa mbaya,” alisema.
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Laptop City

Tangazo