Leonce Zimbandu
Kamanda Simon Sirro |
JESHI la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam
limekanusha taarifa za wizi kwenye Ofisi ya Mpiga Chapa Mkuu wa Serikali likisema
zilikuwa njama za wafanyakazi wa ofisi hiyo.
Tamko hilo lilitolewa jana na Jeshi hilo baada ya kufanya
uchunguzi na kubaini kuwa wizi huo ulisababishwa na vibaka waliokamatwa na
kufikishwa kwenye vyombo vya sheria.
Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam,
Simon Sirro, alisema hayo alipozungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam.
Alisema baada ya Jeshi hilo kupata taarifa, lilifanya
uchunguzi uliosaidia kukamatwa vibaka wanne wakiwa na televisheni, kisimbuzi
cha StarTime na kompyuta mpakato.
“Tumepata vifaa zilivyoibiwa, hivyo wizi huo ulifanywa na
vibaka na si wafanyakazi kama mitandao ya kijamii ilivyoripoti,” alisema.
Alisema tukio hilo lilitokea Novemba 25 mwaka jana usiku
wakati vibaka hao walipoingia kwenye ofisi hiyo kupitia kwenye paa.
Baada ya kuingia waliiba simu, kisimbuzi, kompyuta
mpakato na televisheni na kuondoka, hivyo polisi walipofika eneo hilo, walikamata
walinzi wa zamu ya siku ya tukio kwa ajili ya upelelezi.
Alisema taarifa kamili atazitoa baada ya kukamilisha
upelelezi wa kuwabaini watuhumiwa wote waliohusika na tukio hilo, na kwamba wafanyakazi
wa Serikali hawakuhusika na tukio hilo la kihalifu.
0 comments:
Post a Comment