Edith Msuya
Dk Hamis Kigwangala |
SERIKALI inaanza kufanya utafiti
kuruhusu taulo za wanawake (pedi) ambazo zitakuwa na uwezo wa kutumika mara
mbili kwa wanawake ili ziingie nchini zitumike kwa wanawake na watoto wa kike kujihifadhi.
Akizungumza juzi kupitia kituo kimoja
cha televisheni nchini, Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee
na Watoto Dk Hamisi Kigwangalla alisema kufanyika kwa utafiti huo kunawezesha kuangalia
usalama kwa watumiaji kiafya.
Kwa kauli hiyo gazeti hili lilitafuta
baadhi ya wateja ili kutoa maoni yao ambapo walisema kama zitakuwa na usalama itakuwa
vizuri.
Mmoja wa wafanyabiashara wa Posta,
Mwanaheri Jumaa, alisema utafiti huo ukitoa majibu mazuri na Serikali ikaruhusu
hakutakuwa na tatizo kwa watumiaji.
"Mimi naunga mkono kama zitakuwa na
usalama kwani litakuwa jambo jema kwani usalama ni kitu muhimu," alisema.
Joyce Kimweri alisema kupatikana kwa
pedi hizo ni msaada mkubwa kwa wanawake hasa waishio vijijini.
Alisema wanawake wengi wa vijijini ni vigumu
kwao kuzipata na hata kama wakizipata huwawia vigumu kurudia kuzinunua.
Hamida Shabani alisema ni mpango mzuri
kwa Serikali kwani utakuwa msaada mkubwa hasa kwa watu wa hali ya chini.
"Ni mpango mzuri ila tunachoomba
utafiti unaofanyika ufanyike katika mazingira mazuri bila kusababisha matatizo na
maambukizi kwa mtumiaji," alisema.
0 comments:
Post a Comment