Grace Gurisha
MFANYABIASHARA maarufu Dar es Salaam Hussein Ndama,
maarufu kama ‘Ndama Mtoto wa Ng’ombe (44)’, ameitaka Serikali imweleze
upelelezi wa kesi yake utachukua muda gani kukamilika.
Ndama alitaka kujua hilo kwa kupitia Wakili wake, Wabeya
Kundya ambaye aliliwasilisha ombi hilo jana mbele ya Hakimu Mkazi, Victoria
Ngongwa wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam, baada ya Wakili wa
Serikali, Christopher Msigwa kudai kuwa upelelezi haujamakilika.
Baada ya kutolewa kwa maelezo hayo, Kundya alidai kuwa
ili haki ionekane inatendeka, ni pamoja na kesi kusikilizwa kwa wakati na
akaomba kujua upelelezi utachukua muda gani kukamilika, ambapo Msigwa alidai mwathirika
mmoja wa tukio hilo, yuko nje ya nchi na ana baadhi ya nyaraka.
Hivyo wanafanya naye mawasiliano ili kuona kama anaweza
kuziwasilisha kwa kuzituma au kufika mwenyewe. Kutokana na maelezo hayo, Hakimu
Nongwa aliiahirisha kesi hiyo hadi Januari 19.
Mshitakiwa alirudishwa rumande kwa sababu moja kati ya
mashitaka yanayomkabili la kutakatisha fedha halina dhamana.
Ndama anadaiwa kuwa Februari 20, 2014 Dar es Salaam, alighushi
nyaraka za kibali cha kusafirisha madini na sampuli za madini kwa kusudi la
kuonesha kuwa kampuni ya Muru Platnum Tanzania Investment Limited iliruhusiwa
kusafirisha makasha manne ya dhahabu yenye kilogramu 207 na thamani ya dola 8,280,000
za Marekani kwenda Australia kwenye kampuni ya Trade TJL DTYL Limited wakati
akijua si kweli.
0 comments:
Post a Comment