Peter Akaro
BOHARI
ya Dawa (MSD) imesema upatikanaji wa dawa nchini unatarajiwa kuwa kati ya
asilimia 86 hadi 90 kwa Januari hadi Machi.
Akizungumza
jana Dar es Salaam, Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Laurean Bwanakunu alisema baada ya
kuwasili kwa awamu mbili za dawa kutakamilisha aina 100 za dawa kati ya 135
muhimu.
Bwanakunu
alisema Serikali ilifanya uchunguzi kwenye kitengo hicho ili kuboresha huduma
na kubaini mambo kadhaa ambayo ndiyo yamefanyiwa kazi.
Mambo
hayo ni ufinyu wa bajeti, kuangalia kama sheria iliyoanzisha MSD mwaka 1993 inasadia
utendaji na shughuli, upanuzi wa wigo wa mikataba, kuboresha taratibu za malipo
kwa wazabuni na kuboresha njia za kupata fedha tofauti na zilizopo sasa.
Alisema
MSD imeachana na mpango wa kukodi maghala ya kuhifadhi dawa ambayo yalikuwa
yanawagharimu Sh bilioni nne, ila sasa wameanza ujenzi wa ghala katika kiwanja cha
Luguruni, Ubungo kwa kanda ya Dar es Salaam.
Alisema
pia MSD imeanza utaratibu wa kununua dawa na vifaatiba moja kwa moja kutoka kwa
wazalishaji, utaratibu unaopunguza gharama za ununuzi wa dawa na vifaatiba
kutoka kwa wafanyabiashara.
“Hadi
sasa MSD imetoa mikataba 58 ya ununuzi wa dawa muhimu, na imetangaza zabuni
ambayo itafunguliwa Januari 28, tunatafuta walizashaji 76 wa dawa na 79 wa
vifaa,” alisema.
Alisema
MSD inaendelea na huduma maalumu kwa wateja wake wakubwa ili kuwawezesha kupata
huduma kwa haraka zaidi, wateja hao ni hospitali za Muhimbili, Kibong’oto,
Mirembe, Amana, Temeke, Mwananyamala na KCMC.
Pia
kuna Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Mbeya, Benjamin Mkapa ya Dodoma na Taasisi
ya Moyo ya Jakaya Kikwete.
Kwa
sasa MSD ipo katika mchakato wa kuanzisha viwanda vya kuzalisha dawa na vifaatiba
kupitia mpango wa ushirikishaji sekta binafsi.
Aliongeza
kuwa mwaka jana MSD ilifungua maduka sehemu mbali mbali nchini kwa lengo la kuwezesha
hospitali.
Maduka
ambayo hadi sasa yamefunguliwa ni la Muhimbi, Mount Meru, Arusha; Sekou Toure,
Mwanza; Mbeya; Chato, Geita na Rungwe, Lindi.
“Kwa
sasa tuko mbioni kufungua duka la Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda, Katavi,”
alisema.
0 comments:
Post a Comment