Gwajima ana kesi ya kujibu


Grace Gurisha

Josephat Gwajima
ASKOFU Mkuu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima, ana kesi ya kujibu katika kesi inayomkabili ya kutohifadhi bastola sehemu salama.

Hiyo ilibainika jana baada ya Mahakama kupitia mashahidi watano wa upande wa Jamhuri.

Uamuzi huo ulitolewa na Hakimu Mkazi Mfawidhi Cyprian Mkeha wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam, ambapo alisema Gwajima na wenzake watatu watatakiwa kujibu mashitaka yanayowakabili baada ya kupitia ushahidi.

Wakili wa washitakiwa hao, Peter Kibatala alidai kuwa watakuwa na mashahidi watatu wakijumuishwa na washitakiwa, watakuwa saba, ambapo wote wanne watajitetea chini ya kiapo.

Awali, Mpelelezi wa Ofisi ya Mkuu wa Upelelezi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Sajini Albogast alidai kuwa wasaidizi wa Askofu Gwajima walimpelekea bastola saa nane usiku hospitalini TMJ alikokuwa amelazwa baada ya kuanguka akiwa kituo cha Polisi akihojiwa.

Shahidi huyo alitaja wasaidizi hao kuwa ni Yekonia Bihagaze, George Mzava na Geofrey Milulu, ambao walitenda kosa hilo kinyume cha sheria kwa sababu kwa hali ya kawaida, haiwezekani mgonjwa kupelekewa silaha.

Alidai kuwa Mkuu wa Upelelezi wa Kinondoni alimuunganisha na Mkuu wa Kituo cha Kawe, Pamphil ambaye alimkabidhi begi lililokuwa na silaha bastola namba CAT 5802, risasi tatu zilizokuwa kwenye magazini, CD mbili, risasi 17 za bastola na kitabu cha umiliki wa silaha, nguo ya ndani na hati ya kusafiria ya Mchungaji huyo.
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Laptop City

Tangazo