‘Kuchangia damu hakuna madhara’


Abraham Ntambara

WANANCHI wametakiwa kuacha dhana potofu ya kuamini kuwa mtu anapochangia damu inampasa kufanya hivyo kila wakati kutokana na kwamba atakuwa ukiongezeka damu mwilini kupita kiasi mara kwa mara.

Kauli hiyo ilitolewa mwishoni mwa juma jijini Dar es Salaam na Ofisa Uhamasishaji wa Mpango wa Taifa wa Damu Salama Kanda ya Mashariki, Desteria Nanyanga.

Alisema dhana hiyo ni moja ya changamoto ambayo wamekuwa wakikabiliana nayo.

“Tumekuwa tukikabiliana na changamoto hii. Watu wanaamini ukichangia damu leo, itakubidi kuchangia kila wakati kwa sababu usipofanya hivyo, utapatwa na matatizo kama ya kuumwa kichwa. Leo hii naomba niwaambie hiyo dhana ni potofu,” alisema Nanyanga.

Alifafanua kuwa wanapokuwa wakipita maeneo mbalimbali nchini katika kuhamasisha watu kujitolea kwenye zoezi la uchangiaji wa damu, wananchi wamekuwa wakihofia kuwa wakifanya hivyo itawabidi suala hilo liwe endelevu, kwani kutokufanya hivyo kutawaletea tatizo la kuongezeka damu.

Nanyanga aliongeza kwamba kutokana na hali hiyo watu huamini kwamba unapochangia damu leo itatakiwa kuchangia tena kila baada ya mwezi mmoja au miwili kitu ambacho siyo sahihi.

Alikanusha kwamba siyo kweli kwamba ukichangia damu itabidi iwe hali endelevu kwa maisha yako yote kwa kufanya hivyo, bali unaweza kuchangia kwa hiari yako tu.

Alieleza kuwa kutokana na maumbile ya kibaolojia, mwanaume anaweza kuchangia damu kila baada ya miezi mitatu, huku mwanamke akitakiwa kuchangia damu yake kwa hiari kila baada ya miezi minne.

Alisema kuwa mtu anapaswa kuonana na daktari wa masuala ya damu ili aweze kujua kwa nini chembe chembe zake za damu zinazalisha damu kupita kiasi ili apatiwe matibabu.

Aidha katika kuthibitisha hilo alisema kwa upande wake hadi sasa anatakribani mwaka mmoja na nusu tangu alipochangia damu ambapo alibainisha kuwa hadi leo hajachangia tena na hakuna mabadiliko yoyote anayoyaona katika mwili wake.





Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

1 comments:

  1. Kuna uhusiano gani kati ya uchangiaji damu wa mara kwa mara na matatizo ya moyo?

    ReplyDelete

Laptop City

Tangazo