Zitto: Watanzania someni vitabu


Celina Mathew

Zitto Kabwe
MBUNGE wa Kigoma Mjini (ACT-Wazalendo), Zitto Kabwe ametaka Watanzania wajiwekee utaratibu wa kusoma vitabu huku akibainisha kuwa mwaka huu alisoma vitabu 53, idadi aliyodai kuwa hakupata kuifikisha huko nyuma.

Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari, Zitto alisema aliamua kusoma idadi hiyo ya vitabu mwaka huu ili mwakani apate wakati mzuri wa malezi baada ya mkewe kujifungua.

"Mwaka huu nimeongeza idadi ya vitabu nilivyosoma tofauti na mwaka jana, lakini sikufikia idadi ya mwaka juzi ambapo nilisoma 56. Hiyo ndiyo rekodi ya juu zaidi tangu nilipoanza kuorodhesha vitabu nilivyosoma mwaka 2012. Mwaka 2013 niliorodhesha vitabu vichache zaidi," alisema.

Alisema mwaka huu ulimfunua kuhusu uwezo mkubwa na umahiri wa wachapishaji wa vitabu wa ndani na kwamba alipata fursa adhimu ya kuzungumza na Walter Bgoya wa kampuni ya uchapishaji ya Mkuki na Nyota.

Alisema alijifunza mengi mapya ya historia ya nchi na Afrika na kwamba kisa kilichomchekesha ni anapokumbuka hadithi ya Rais Seretse Khama wa Botswana alivyobeba machungwa kwenye ndege kumletea zawadi Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere akimtania kuwa sera zake za Ujamaa zilileta njaa nchini.
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Laptop City

Tangazo