Mahakama yakwama kutoa uamuzi kesi ya mauaji


Grace Gurisha

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam imeshindwa kutoa uamuzi wa kama itafuta mashitaka ya mauaji dhidi ya mke wa marehemu bilionea Erasto Msuya, Miriam Msuya (41) anayetuhumiwa kumuua dada wa marehemu, Aneth.

Hiyo inatokana na Mahakama hiyo jana kukwama kutoa uamuzi, ikiwa ni mara kadhaa sasa tangu Agosti 10 ilipotakiwa ifanye hivyo kwa mara ya kwanza.

Hakimu Mkazi, Magreth Bankika amekuwa akiiahirisha kesi hiyo mara kadhaa na baadaye kuihamishia Mahakama nyingine ambako ilipangiwa Godfrey Mwambapa, lakini bado uamuzi haujatolewa kila ikija inaelezwa kuwa bado uamuzi haujakamilika.

Kesi hiyo ilikuja jana mbele ya Hakimu Mwambapa, ambapo aliahirisha hadi Desemba 29 atakapotoa uamuzi.

Hatua hiyo ilifikiwa na Mahakama hiyo, baada ya Wakili wa Miriam, Peter Kibatala kuwasilisha ombi hilo mbele ya Hakimu Mkazi Magreth Bankika kuwa hati ya mashitaka ina kasoro na kuomba ifutwe pia akidai kuwa wateja wake waliteswa na polisi.

Mbali na Miriam, mshitakiwa mwingine ni mfanyabiashara wa Arusha, Revocatus Muyela (40), ambapo Kibatala alidai pia kuwa washitakiwa hao waliteswa na askari kabla ya kuchuliwa maelezo, ili wakiri kuhusika na mauaji hayo.

Akijibu hoja hizo, Wakili wa Serikali, Diana Lukondo alifdai hati ya mashitaka iliyo mahakamani hapo iko sahihi kwa kuwa ina sababu zote za kuitwa hati ya mashitaka, kwa hiyo hoja za Kibatala hazina mashiko.

Muyela aliunganishwa katika kesi hiyo, baada ya kukamatwa na kubainika kuwa anatuhumiwa na mauaji hayo. Aneth ni dada wa marehemu bilionea Msuya, na alichinjwa na watu wasiojulikana nyumbani kwake Kibada, Block 16, Kigamboni, Dar es Salaam Mei 26.
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Laptop City

Tangazo