Tanzania, Kenya waunda tume kusimamia ajira


Venance Nestory

Balozi Augustine Mahiga
TANZANIA na Kenya wametia saini ya uundwaji wa Tume ya pamoja itakayoleta maboresho katika mazingira ya uwekezaji, biashara na kuongeza fursa za ajira kwa vijana baina ya nchi hizo mbili.

 Utiaji saini huo ulifanywa mwishoni mwa wiki kati ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Tanzania, Balozi Augustine Mahiga na Waziri wa Mambo ya nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Kenya, Balozi Amina Mohamed.

Awali, marais wa nchi hizo Uhuru Kenyata (Kenya) na Rais John Magufuli, walikutana na kukubaliana kuendeleza kukuza uhusiano wao ambao ulianzishwa tangu enzi wa waasisi wa nchi hizo mbili.

Katika mkutano wa tatu wa Tume ya pamoja ya Ushirikiano, walikubaliana katika sekta ya Nyumba na Maendeleo ya vijiji, Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (ICT), Uvuvi, Mazingira, Usafiri wa mjini na Sekta ya Nishati na Madini.

Pia, mkutano huo uliamua kuweka mfumo wa ufuatliaji wa karibu wa makubaliano hayo yaliyofikiwa chini ya Makatibu Wakuu wa Wizara za Mambo ya Nje ya nchi hizo. Chombo hicho kitakuwa kikikutana kila baada ya miezi sita.

Wachambuzi wameeleza kuwa makubaliano hayo yataleta msukumo mpya baina ya nchi hizo mbili katika kuimarisha urafiki wake na kukuza dhana ya ujirani mwema.

Tanzania na Kenya ikakubaliana kuendeleza ushirikiano wao katika Jumuiya ya Afrika Mashariki, Umoja wa Afrika na Umoja wa Mataifa katika kujikwamua kiuchumi na maendelea ya nchi hizo mbili.
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Laptop City

Tangazo