Polisi Tanga watoa orodha ya wahalifu


Mariam Cyprian, Tanga

JUMLA ya kesi 20,601 zimeripotiwa mkoani hapa katika kipindi cha  Januari hadi Novemba, ikiwa ni pungufu kwa kesi 565 ikilinganishwa na kesi 2016 zilizoripotiwa mwaka 2015.

Takwimu hizo zilitolewa na Kamanda wa Polisi mkoani Tanga, Benedict Wakulyamba wakati akitoa taarifa ya hali ya usalama kwa waandishi wa habari ofisini kwake.

Wakulyamba alisema kuwa kati ya kesi hizo 20,601 zilizofunguliwa, Jumla ya kesi 7,056 zilifikishwa mahakamani na kesi 2,198 washtakiwa wake walitiwa hatiani na kupewa adhabu mbalimbali.

Alisema wastakiwa wa kesi 1,472 waliachiwa huru na Mahakama kwa sababu za kisheria. “Kesi nyengine ziko katika hatua mbalimbali za uendeshaji.

Aidha Kamanda huyo alisema kuwa katika kipindi hicho Jeshi la Polisi liliendesha misako na operasheni mbalimbali na kufanikiwa kukamata wahalifu waliofanya au kutaka kufanya vitendo vya uhalifu ikiwa ni pamoja na vielelezo mbalimbali vya kesi zao.

Akizungumzia kwa upande wa wahamiaji katika kipindi hicho alisema walikamata wahamiaji haramu 168; kati yao wahamiaji 73 Wasomalia, kumi Waethiopia na wengine Wakenya.

Aidha kwa upande wa madawa ya kulevya, kamanda huyo alisema kesi za bangi 294 zilifunguliwa kwenye vituo vya Polisi ambapo Bangi yenye uzito wa kg 1,188.2 ilikamatwa na kulikuwa na kesi 165 za mirungi

 “Lakini pia kwa upande wa madawa ya kulevya ya viwandani jumla ya kesi 54 zilifunguliwa, zikihusisha kukamatwa kwa jumla ya gramu 130.48 za madawa ya kulevya,” alisema RPC huyo.

Hata hivyo, Kamanda huyo alisema pia katika kipindi hicho walifanikiwa kukamata silaha za moto 37 katika kupambana na uzibiti wa matukio ya ujambazi na unyang’aji kwa kutumia silaha ikiwa ni mkakati wa kukabiliana na vitendo vya uhalifu mkoani hapa ili kuhakikisha vinamalizika.

Sambamba na hilo lakini pia Jeshi hilo lilifanikiwa kukamata risasi   ambapo kati ya hizo risasi 425 zilikuwa za SMG,Risasi 24 zilikuwa za  Shotgun na Risasi 25 zilikuwa ni za Rifle.

Alisema kuwa katika kipindi hicho silaha ambazo zimekamatwa ni SMG  nane,Marker IV mbili,Shotgun nne,Pistol moja  na Rifle mbili ambazo  zilikamatwa kwenye matukio mbalimbali yaliyokuwa yakitokea mkoani  hapa.

Aidha alisema katika ya silaha hizo pia mabomu manne ya kurusha kwa  mkono na Gobore ishirini zilikamatwa kwa watuhumiwa wa uhalifu mkoani hapa ambayo yalikuwa yakitumika kufanyia vitendo vya uhalifu.

"Katika kipindi hicho tuliweza kukamata risasi 425 za SMG, risasi 24 za shotgun na risasi 25 za rifle zilizokamatwa kutokana na misako mbalimbali iliyofanywa na Jeshi la Polisi kwenye matukio mbalimbali,” alisema RPC Wakulyamba.
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Laptop City

Tangazo