Mvua yaharibu makazi Kalombo


Ibrahim Yassin

WAKAZI wa kijiji cha Kateka kilichoko katika Kata ya Matai wilayani Kalambo wameingia kwenye wakati mgumu baada ya makazi yao kuharibiwa na mvua kubwa iliyokuwa imeambatana na upepo mkali.

Mvua hiyo imeezua mapaa ya nyumba 17 na kufanya wakazi wake wakose makazi katika kipindi hiki cha mvua za masika.

Wakizungumza na gazeti hili huku wakilia, baada ya kutokea kwa adha hiyo walisema mvua hiyo iliyonyesha ghafla, imefanya uharibifu mkubwa katika eneo hilo.

Juma Mwanalinze alisema kuwa mvua hiyo ilinyesha kwa muda wa dakika thelathini tu lakini imefanya uhalibifu mkubwa.

Wakazi hao wameiomba Serikali kuwasaidia kupata mahala pa kujihifadhi katika kipindi hicho cha mvua, kwani hawana na namna ya kufanya kwa ajili ya kujisiri.

Afisa tarafa ya Matai, Andrew Manyema Ngindo, licha ya alisema baada ya kutokea adha hiyo walitoa taarifa kwa mkuu wa wilaya hiyo, Julieth Binyura samba samba na kutoa taarifa kwenye uongozi wa halmashauri husika.

Alisema viongozi wote walifika eneo la tukio na kushuhudia zaidi ya kaya kwenye eneo hilo zikiwa zimehalibiwa vibaya na kusema mpaka sasa kamati ya maafa imekaa ili kutathmini watu walioathirika na janga hilo na kuangalia namna ya kuwasaaidia.

Alisema chanzo ni kutokana ni wananchi wengi kujenga nyumba zisizo kuwa imara.

Mkuu wa wilaya hiyo, Julieth Binyula alisema ameanza ziara ya kuangalia maeneo yote yaliyokubwa na kadhia hiyo na kuahidi kutoa taarifa zaidi, baada ya kumaliza uchunguzi na kufanya tathmini kwa wathirika wote.

Alisema ipo haja ya wananchi kupanda miti kwa wingi ili kuzuia upepo unaoharibu makazi na kuwa makazi mengi yameharibiwa kutokana na maeneo mengi kutokuwa na miti.
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Laptop City

Tangazo