Kesi ya Lissu kuanza Januari 18


Grace Gurisha

KESI ya uchochezi inayomkabili Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu (Chadema) na Mhariri wa gazeti la Mawio, Simon Mkina inatarajia kuanza kusikilizwa Januari 18, 2017 baada ya upelelezi wa kesi hiyo kukamilika.

Washitakiwa wengine katika kesi hiyo ni Jabir Idrisa na Mchapishaji wa Kampuni ya Jamana, Ismail Mehboob.

Upande wa Jamhuri ulidai jana mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi Thomas Simba kuwa kesi ilikuja kwa kusikilizwa, lakini hawana mashahidi kwa hiyo wanaomba wapangiwe tarehe nyingine ya kuendelea kusikiliza kesi hiyo.

Hakimu alikubaliana na ombi hilo na kuahirisha kesi hiyo hadi mwakani, ambapo washitakiwa hao waliwakilishwa na Peter Kibatala. Awali, hakimu huyo alishangaa upande wa Jamhuri kushindwa kumkamata Lissu licha ya kwamba yeye alitoa hati ya kukamatwa kwa Mbunge huyo.

Hata hivyo, alimueleza Lissu kuwa aachane na mambo anayofanya kwa sababu yeye ni kioo cha jamii, kwa hiyo hastahili kufanya anayoyafanya na pia yeye ni mwanasheria na ajua sheria.

Ilidaiwa Januari 12 hadi 14, 2016 katika jiji la Dar es Salaam, washtakiwa watatu, Jabir, Mkina na Lissu, kwa pamoja waliandika na kuchapisha taarifa? za uchochezi zenye kichwa cha habari kisemacho, ‘Machafuko yaja Zanzibar’.
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Laptop City

Tangazo