TPSF yajizatiti kuwawezesha vijana


Emeresiana Athanas

TAASISI ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), imesema inatarajia kuanza utekelezaji wa utoaji wa elimu ya ujasiriamali kwa watumishi wa umma ili waweze kuanzisha biashara watakapo staafu.

Aidha inatarajia pia kutoa elimu ya ujasiriamali kwa vijana, mradi ambao utasaidia kutokomeza suala la ukosefu wa ajira kwa vijana  kwa kuimarisha utendaji uliosheheni uadilifu.

Akizungumza Dar es Salaam jana wakati wa hafla ya kumtambua mjasiriamali mahiri wa mashindano ya Ujasiriamali Barani Afrika Jenifer Shigholi, Mwenyekiti wa Bodi ya TPSF, Salum Shamte alisema kuwa watumishi wa umma wakiandaliwa vizuri watachangia maendeleo ya taifa kutokana na upeo wako kuwa mkubwa.

"Elimu hii itawapa uwezo kwa kutumia mbinu mbalimbali kwa kuanzisha biashara watakazoweza kusimamia, kuziendesha na kuwaletea maisha bora," alisema.

Kuhusu vijana alisema kuwa elimu hiyo itampa mbinu bora ya matumizi ya fedha na rasilimali mbalimbali ili aweze kujiajiri wenyewe na kutengeneza ajira kwa wenzao.

"TPSF kwa kushirikiana na Wizara ya Kazi, Ajira, Sera na Walemavu iko mbioni kukamilisha programu ya mafunzo ya kazi ya awali inayolenga vijana wahitimu ili waweze kupata ujuzi wakati wanasubiri kupata ajira," alisema.
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Laptop City

Tangazo