Abdulrazak, Juma kuchuana ubunge Dimani


Mwandishi Wetu, Zanzibar

Maalim Seif
MAJINA ya wagombea ubunge katika Jimbo la Dimani kutoka Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Chama cha Wananchi (CUF) yametangazwa.

Mgombea wa CUF ni Abdulrazak Khatib Ramadhan na wa CCM ni Juma Ali Juma na wote wamesema wako tayari kwa kampeni zinazoanza kesho.

Naibu Katibu Mkuu wa CUF Zanzibar, Nassor Ahmed Mazrui, aliiambia JAMBOLEO juzi kuwa Baraza Kuu la CUF lilimteua Ramadhan kuwania ubunge wa Dimani.

“Jumapili mgombea tuliyempitisha alichukua fomu ya uteuzi kwenye ofisi ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Wilaya ya Magharibi B,” alisema Mazrui.

Mgombea wa CCM naye alichukua fomu kwenye ofisi za muda za NEC katika sekondari ya Kiembe Samaki na sasa wanasubiri uchaguzi pekee.

Mbali na uchaguzi mdogo wa ubunge Dimani pia NEC itaendesha uchaguzi wa udiwani kwenye kata 22 nchini ambapo jumla ya Sh.  bilioni tatu zitatumika.

Mkurugenzi wa Uchaguzi wa NEC, Ramadhan Kailima alisema maandalizi ya uchaguzi huo yamekamilika, ambapo Sh bilioni 1.7 zitatumika kwenye uchaguzi mdogo wa Dimani na Sh bilioni 2.2 zitatumika kwa uchaguzi wa udiwani kwenye kata 22.

Fomu zilianza kutolewa Desemba 15 ambapo mwisho itakuwa ni Desemba 22 na kampeni zitaanza rasmi Desemba 23 hadi Januari 21.

Uchaguzi mdogo wa Dimani unafanyika kutokana na kifo cha Hafidh Ali Twahir aliyefariki dunia  Novemba 11 kwenye hospitali ya rufaa ya Dodoma.
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Laptop City

Tangazo