Wazazi wa watoto watakaopotea kushitakiwa


Salha Mohamed

Advera Bulimba
JESHI la Polisi limesema litawakamata wazazi wa watoto watakaopotea wakati wa Sikukuu za Krismasi na Mwaka Mpya kwa kushindwa kutekekeza majukumu yao.

Hatua hiyo imedaiwa ni kushindwa kutekeleza majukumu yao huku watoto wakijaa katika vituo vya Polisi kutokana na kupotea.

Akizungumza jana Dar es Salaam, Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini, Advera Bulimba, alisema Jeshi hilo halitawavumilia wazazi wa watoto watakaopotea nyakati hizi za sikukuu.

“Utakuta watoto wanajaa kwenye vituo vya Polisi kwamba wamepotea…sasa tunajiuliza amepotea mzazi wake alikuwa wapi? Lazima mzazi awajibike na tutamchukua mzazi aweze kuisaidia Polisi kutwambia kwa nini mtoto wake amefika kituo cha Polisi yeye alikuwa wapi,” alisema.

Bulimba ambaye pia ni Kamishna Msaidizi wa Jeshi hilo, alisema katika sikukuu hizi wazazi wanakuwa na tabia ya kuacha watoto wao na kwamba wanakwenda kwenye starehe kama fukweni na kutembea wenyewe jambo ambalo hawatakubaliana nalo.

Alisema wazazi hao wataisaidia Polisi kufanya uchunguzi kwani kupotea kwa watoto ni uzembe.

Bulimba aliwataka wananchi kuwa makini katika kipindi hiki, kwani kuna matapeli wanaotumia majina ya viongozi kutaka taarifa zao au fedha kutoa taarifa Polisi.

“Hatutawavumilia wanakunywa pombe na kuendesha magari tutawachukulia hatua za kisheria, wamiliki wa kumbi za starehe wazingatie uhalali wa leseni zao katika uingizaji watu,” alisema.

Bulimba aliongeza kuwa ni vema wamiliki wa maduka na hoteli kufunga vifaa vya kufuatilia taarifa za wateja wao (kamera) ili kufuatilia nyendo zao.

Alitaka wananchi wanapoona watu tofauti na mazingira wanamoishi watoe taarifa Polisi au kumtambua mhusika asiyefahamika.

Alisema “wananchi wakishirikiana tunaweza kupata taarifa za kihalifu mapema na kuudhibiti, na hata wafanyabiashara wa maduka hufanya hivyo,” alisema.

Alitaka wananchi kuwa makini na hata kutoa taarifa za askari wazembe wanaochelewesha kutoa huduma kwa wananchi kwani zipo taratibu za kuwawajibisha kwani wasiofanya kazi kwa weledi.

“Kuna vituo vinahamishika hivyo ni kuhakikisha kwamba mwananchi anapata huduma haraka na kwa wepesi kama kuna taarifa zozote waseme,” alisema.
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Laptop City

Tangazo