Yaliyotikisa Mkoa wa Arusha 2016


Richard Mwangulube

MKOA wa Arusha katika mwaka wa 2016 umetikiswa na mambo mkubwa matano, ikiwamo  mbunge wa Jimbo la Arusha  Godbless Lema kuingia katika mgogoro na Serikali na kulazimika  kufikishwa mahakamani mara kadhaa.

Mbunge huyo amelazimika kukwama kutoka rumande kwa kipindi kirefu kutokana na lugha zake tata kwa viongozi wa Serikali wa wilaya na mkoa.

Mara kadhaa Lema ameshindwa kupata dhamana mahakamani kwa takribani zaidi ya mwezi tangu alipofikishwa mahakamani kwa mara ya kwanza.

Jambo lingine ambalo lilitikisa mkoa huo na taifa kwa ujumla ni utata wa Faru John  kama  ilivyoanishwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa  alipotembelea mamlaka ya hifadhi ya Ngorogoro. Faru John amezua utata mkubwa  serikalini na wizara husika  ya Maliasili na Utalii.

Jambo jingine  ambalo limeutikisa mkoa na taifa pamoja na tasnia ya habari nchini kote  ni la kuwekwa rumande mwandishi wa habari wa redio one na ITV,  Khalfan Liundi kwa amri ya Mkuu wa Wilaya ya Arumeru  Alexander Mnyeti.

Liundi anadaiwa kuwa alikwenda katika vijiji vya wilaya ya Arumeru na kuandika habari za uchochezi. hatua hiyo imedaiwa na mkuu huyo wa wilaya kuwa ni kuingilia uhuru wa habari.

Mkoa wa Arusha katika mwaka huu wa 2016 pia umetikiswa na kuzuka kwa ugonjwa hatari wa Kimeta (ANTHRAX) ambao umeua wanyamapori wengi katika Wilaya ya Monduli.

Ugonjwa huu mbali na kuua wanyamapori na mifugo pia uliathiri sekta ya utalii katika kipindi kifupi tangu uzuke.

Sekta ya utalii ilitikiswa zaidi katika hifadhi ya Manyara katika Vijiji vya Selela hali ambayo ilipunguza idadi ya watalii waliotembelea baadhi ya vivutio katika hifadhi ya Manyara.

Katika kukabiliana na ugonjwa huu Wataalam kutoka taasisi mbalimbali zinazohusiana na sekta ya wanyamapori na mifugo kulazimika kutumwa katika wailaya ya Monduli ili kudhibiti ugonjwa huo
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Laptop City

Tangazo