Chadema wakutana kwa dharura


Celina Mathew

SEKRETARIETI ya Chadema, imefanya kikao cha dharura kujadili masuala mbalimbali likiwamo la Rasimu ya Katiba.

Kutokana na kikao hicho, Baraza la Vijana la Chadema (Bavicha), liliahirisha mkutano wake uliokuwa ufanyike jana na badala yake utafanyika leo.

Akizungumza na JAMBO LEO, Msemaji wa Chama hicho, Tumaini Makene alisema Sekretarieti hiyo lengo lake ni kusimamia utendaji wa chama na vikao vyake hufanyika siku yoyote, muda wowote.

Alisema kwenye kikao hicho pamoja na kuzungumzia masuala ya chama pia ajenda nyingine inaweza kuwa maandalizi ya vikao vya ndani vya chama vyenye lengo la kujadili Rasimu ya Katiba ya Jaji mstaafu Joseph Warioba.

Kikao hicho kilifanyika chini ya Katibu Mkuu wa Chama, Dk Vincent Mashinji, manaibu wake, wakurugenzi wote wa chama na wataalamu wengine kwa mujibu wa Katiba ya Chama.
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Laptop City

Tangazo