Manispaa Ilala yagoma kuingia mgogoro wa ardhi



MANISPAA ya Ilala imegoma kuingilia kati mgogoro wa viwanja unaofukuta baada ya halmashauri hiyo kuimilikisha Kampuni ya Green Foundation, kabla ya wakazi wa eneo hilo kulipwa fidia, akiwamo Said Andanenga na wenzake.

Kauli hiyo ilitolewa na Mkuu wa Idara ya Ardhi na Upimaji wa Manispaa ya Ilala, Paul Mbembela alipokuwa akizungumza na gazeti hili jijini Dar es Salaam jana.

Alisema manispaa haijasaini mkataba wa upimaji wa viwanja na wananchi, bali iliingia mkataba na Kampuni ya Green Foun-dation baada ya kupitia vielelezo vilivyowasilishwa ofisini kwake.

“Unajua kampuni ilifuata taratibu zote ikiwamo barua ya serikali ya Mtaa wa Mbondole, hivyo kama manispaa ilimpatia umiliki katika eneo hilo,” alisema.

Alisema ikiwa wananchi watakuwa na vielelezo vya Green kukiuka mkataba wao, wanapaswa kutoa malalamiko yao man-ispaa ili yashughulikiwe kwa mujibu wa taratibu.

Awali, mmoja wa wakazi hao, Andanenga ambaye pia ni mwanachama wa Green Foundation alisema yeye kwa niaba ya wenzake aliandika barua mara tatu na kuzipeleka ofisi ya manispaa, lakini hazikujibiwa.

Alisema mwaka 2007 waliamua kupima eneo hilo chini ya kampuni hiyo na kuahidiwa kupata ofa ya viwanja hivyo, wanashangaa baadhi ya vigogo wa manispaa kugawana viwanja katika maeneo waliyotoa.

“Manispaa haiwezi kukwepa lawama wamehusika kwa asilimia 100 wakishirikiana na Green Foundation kutudhulumu haki zetu,” alisema. Mwenyekiti wa Mtaa wa Mbondole, Thomas Nyanduli, alisema anaufahamu mgogoro huo, lakini anaiomba manispaa kuingilia kati ili kunusuru mapigano.

Alisema hali ni mbaya katika eneo hilo kwani baada ya wananchi kushindwa kupatiwa ofa zao, wameamua kuuza viwanja vya aliyemilikishwa na manispaa.

“Manispaa inapaswa kufika eneo husika kuainisha mipaka, haiwezekani mwenye hati ya kiwanja kumkuta mtu mwingine akijenga kwenye kiwanja, lazima ugomvi utatokea,” alisema.
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Laptop City

Tangazo