Hatuwajui maiti waliozikwa mto Ruvu - Polisi

Salha Mohamed

Kamishna Robert Boaz
WAKATI Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba akidai maiti saba iliyopatikana eneo la Mto Ruvu ni wahamiaji haramu, Jeshi la Polisi limesema halijawafahamu watu hao kwa kuwa linaendelea na upelelezi.

Aidha, limesema linaendelea na upelelezi kuhusu taarifa za kupotea kwa Bernard Focus ‘Saaanane’ ambaye ni mtumishi ndani ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) aliyetoweka Desemba 5 mwaka huu.

Akizungumzia tukio hilo, Kaimu Mkurugenzi wa Upelelezi na Makosa ya Jinai, Kamishna Robert Boaz, alisema Desemba 9 mwaka huu miili hiyo ilikutwa mto Ruvu eneo la Makurunge wilaya ya Bagamoyo.

“Baada ya taarifa hizo kupatikana zilifikishwa kituo cha polisi ambapo polisi na madaktari walifika eneo la tukio na kufanya uchunguzi wa kitaalamu,” alisema.

Alisema miili sita ilionekana kuwa na hali mbaya hivyo waliamua kuizika eneo la tukio, huku maiti moja ikichukuliwa na kupelekwa hospitali ya Wilaya ya Bagamoyo kuhifadhiwa na kufanyiwa uchunguzi na utambuzi zaidi.

Alifafanua kuwa hadi Desemba 16 maiti hiyo haikutambulika na ndipo Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo kuamua kuizika.

“Kumekuwepo na taarifa nyingi kwenye vyombo vya habari na mitandao ya kijamii kudai maiti kuzikwa mapema, huku tukio likiwa halipewi uzito unaostahili,” alisema.

Alisema kuwa wananchi wanapaswa kujua kuwa hatua za kitaalamu zilifuatwa huku wakiendelea kufanya upelelezi unaolenga kuwatambua marehemu pamoja na kujua kilichowasibu.

Wakati huo huo, Kamishna Boaz alisema jeshi linachunguza taarifa ya kupotea kwa kwa mwananchi Focus ‘Saanane’ ambapo jalada la uchunguzi limeshafunguliwa.

“Tunashukuru wananchi ambao wamekuwa pamoja nasi wakitupatia taarifa mbalimbali na tuahidi kwamba taarifa hizo tunazifanyia kazi,” alisema.

Akijibu swali juu ya uwepo wa Saanane katika maiti saba zilizopatikana mto Ruvu, Kamishna Boaz alisema “Sina jibu sahihi kwamba ndiye au siye.”

Kamishna Boaz aliwataka wananchi kuwa watulivu wakati jeshi la polisi linapoendelea na upelelezi kuhusu t ukio hilo.

Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Laptop City

Tangazo