Mwaka mpya kumkuta Lema gerezani


Mery Kitosio, Arusha

MTUHUMIWA wa uchochezi, Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema, ataaga mwaka huu na kukaribisha mpya akiwa gerezani.

Hali hiyo ilijidhihirisha jana baada ya kurudishwa gerezani Kisongo, kutokana na Mahakama Kuu ya Tanzania kanda ya Arusha, kusikilioza hoja za opande mbili kwnye kesi yake na kuamua kutioa uamuzi Januari 4.

Awali Mahakama hiyo ilisikiliza maombi ya notisi ya rufaa yaliyowasilishwa na upande wa Jamhuri na wa mshitakiwa Lema na pande hizo kukubaliana kusikilizwa rufaa ya upande wa Jamhuri huku wa Lema ukiiomba Mahakama kuwasilisha wake kesho kwa maandishi.

Hata hivyo, baada ya kukamilika kwa hoja hizo za kujibizana kwa maandishi ndani ya siku mbili uamuzi wa rufaa hiyo sasa ikaonekana utatolea Januari 4.

Rufaa hizo ni pamoja na ya Jamhuri kutoridhika na uamuzi wa Jaji Dk Modesta Opiyo wa kuwapa siku 10 akina Lema kuwasilisha notisi ya rufaa na upande wa mshitakiwa ni ile ya kupinga uamuzi wa Mahakama ya chini kushindwa kumpa Lema masharti ya dhamana.

Jaji aliyesikiliza rufaa hizo, Salma Magimbi alisema baada ya upande wa Jamhuri kuwasilisha rufaa kwa njia ya maandishi upande wa   Lema utaijibu Desemba 30 huku Januari 2 pande hizo zikikutana kufanya majumuisho na uamuzi wa rufaa hizo kutolewa Januari 4.

Baada ya kusikiliza rufaa hizo, Mahakama iliibua hoja yenyewe na kuwapa kazi mawakili wa pande hizo kuangalia na kutoa hoja kuhusu uhalali kisheria kuhusu notisi iliyotolewa na Serikali kama ilikuwa na mashiko ya kisheria.

Wakili wa mshitakiwa, Peter Kibatala alisema upande wake uliiomba Mahakama kusubirisha rufaa yao ili wasikilize rufaa ya upande wa Jamhuri kwani rufaa zote ziligongana na kuelekea sehemu moja.

"Unajua leo rufaa mbili zimegongana; ya Jamhuri na yetu, hivyo tumeiomba Mahakama isitishe yetu ili isikilizwe ya Jamhuri kwanza, kwani rufaa zote zinaelekea upande mmoja,wa ndege apande ndege na wa basi apande basi, la msingi tunaelekea sehemu moja sote," alisema Kibatala.

Lema alirudishwa tena kwenye gereza la Kisongo hadi Januari 4 Mahakama hiyo itakapotoa uamuzi wa rufaa hiyo.
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Laptop City

Tangazo