Waziri ateua bodi ya Tantrade


Mwandishi Wetu

Charles Mwijage
WAZIRI wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage, ameteua wajumbe tisa wa Bodi ya Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade).

Taarifa kutoka kwa Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Adol Mkenda inaeleza kuwa kufuatia Rais John Magufuli kumteua Christopher Chiza kuwa mwenyekiti wa bodi hiyo, Mwijage ametekeleza wajibu wake wa kuteua wajumbe.

Mkenda aliwataja wajumbe walioteuliwa kuwa ni Dorothy  Mwanyika, Canuth Komba, Leo Mavika,Alfred Mapunda , Francis Lukwaro , Geofrey Kirenga,Mkwale Taib ,Seif Issa,Mohamed  Jumanne.

Alisema uteuzi huo unaanza Desemba 17 Mwaka huu.

Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Laptop City

Tangazo