Chenji yaumiza kichwa mabasi ya haraka


Abraham Ntambara

KAMPUNI ya Mabasi Yaendayo Haraka (UDA-RT) imekiri changamoto ya chenji ya Sh 50 na kusema ufumbuzi wa tatizo hilo ni kutumia kadi za elektroniki.

Akizungumza na JAMBO LEO jana Dar es Salaam Ofisa Uhusiano wa Udart, Deus Buganywa alisema mfumo ulivyo na ulivyoandaliwa unatakiwa kutumia kadi kwa asilimia 90.

“Kwa maana kwamba matumizi ya tiketi yawe kwa asilimia 10 au chini ya asilimia 10,” alisema Buganywa.

Alisema kutumia kadi kutaondoa usumbufu wa watu kukaa kwenye foleni wakisubiri kununua tiketi ambapo alibainisha kuwa pia itakuwa imesaidia kutatua kero ya chenji.

Aliongeza kuwa mtu anapokuwa na kadi huitumia kwa matumizi binafsi kwa sababu inampa fursa ya kulipia nauli hata kwa njia ya simu na hivyo kumwepusha adha hiyo.

Buganywa alisema teknolojia ya kadi lengo mojawapo ni kuondoa kero ya chenji.

Alisema pamoja na tatizo hilo wamejitahidi kukabiliana nalo kwa kutafuta chenji kutoka benki lakini pamoja na juhudi hizo bado tatizo liko pale pale kwa kuwa wanapata chache hivyo hazitoshelezi mahitaji.

Alieleza kwamba wamekuwa wakijitahidi kuzitafuta lakini zinapopatikana zinakuwa chache akibainisha kuwa ili kukabiliana zaidi na tatizo hilo wameanzisha dirisha maalumu la chenji.

Dirisha hilo kazi yake ni kukusanya fedha za mfumo wa chenji zinazoletwa na abiria, ili kusaidia wanaohitaji chenji.
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Laptop City

Tangazo