Wenye kisukari wahimizwa kujiunga na bima ya afya


Abraham Ntambara

WAGONJWA wa Kisukari nchini wameendelea kuhimizwa kujiunga na mifuko ya Bima ya Afya ili kukabiliana na changamoto ya gharama za matibabu.

Mratibu wa Magonjwa yasiyo ya Kuambukiza kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya JamiiJinsia, Wazee na Watoto Dk. Mariam Kalomo alimwambia mwandishi wa habari hii ingawa kwa sasa watoto na watu wa umri chini ya miaka 26 wanapatiwa matibabu bure, wagonjwa wengi bado wanalazimika kulipia huduma hiyo.

“Kama ni mtoto basi yeye anauhakika wa kupata matibabu bure kwenye ile mikoa ambayo ina kliniki kwa sababu zinasaidiwa na shirika la kisukari duniani. Lakini wajiunnge kwenye mifuko ya bima ya afya, sasa hivi wametoa fungu la watoto, ipo ya Sh. 50,000,” Kalomo.

Dk. Kalomo alisema kuwa vipimo kwa wagonjwa wote wa kisukari wamekuwa wakipatiwa bure, isipokuwa dawa hususani kwa watu wazima ndiyo wamekuwa wakilazimika kujinunulia wanyewe.

Aidha alikumbusha kwamba Sera ya Serikali ni kuhakikisha wagonjwa wa magonjwa sugu ikiwa ni pamoja na ugonjwa wa kisukari inatakiwa matibabu yao yawe bure, lakini inabaki kuwa changamoto na kutokidhi mahitaji, hivyo kuwataka watu wazima kujihudumia wenyewe katika matibabu.

Dk. Kalomo aliongeza kuwa Serikali imejipanga vizuri ili kusaidia katika matibabu ya magonjwa sugu kama hayo ndiyo maana Serikali imeongeza fungu katika bajeti ya mwaka 2016/2017 ambayo itasaidia katika ununuzi wa dawa.

Alisema Shirika la Kisukari Duniani (World Diabetes Federation) ndiyo ambalo limekuwa likisaidia kuchangia batibabu ya bure kwa wagonjswa wa kisukari nchini hususani kwa watoto na watu wa chini ya umri wa miaka 26.

Alibainisha kwamba nzima nzima ina kliniki takribani 40 tu zanazotoa huduma ya ugonjwa wa kisukari ambapo alisema zinapatikana kote Tanzania Bara na Visiwani hususani katika hospitali za mikoa na wilaya.

Dk. Kalomo alisema kliniki hizo zimekuwa zikipata misaada kutoka katika Shirika hilo ya dawa, Sirinji pamoja na vifaa vya vipimo vya ugonjwa huo kutoka katika ambavyo vyote, wagonjwa hususani wa watoto na watu wa chini ya umri wa miaka 26 huhudumiwa bure.

Aidha alisema pamoja na shirika hilo kutoa mchango wake nchini bado kuna wakati kuna kuwa na changamoto ya kukosekana kwa dawa hali ambayo hupelekea wagonjwa wanaofaidika matibabu ya bure kulazimika kujinunulia dawa.


Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Laptop City

Tangazo