Rea yapata mwenyekiti mpya wa bodi


Daudi Manongi-MAELEZO

BODI ya Nishati Vijijini (REB), imemteua Boniface Gissima Nyamo-Hanga kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini (Rea) kuziba nafasi iliyoachwa wazi na aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Wakala huo Dk. Lutengano Mwakahesya aliyestaafu mwezi Juni 2016.

Taarifa iliyotolewa na mwenyekiti wa bodi hiyo Dk. Gideon Kaunda ilieleza kuwa uteuzi huo umefanyika kwa mujibu wa Sheria namba 8 ya mwaka 2005 ya Nishati Vijijini katika kikao kilichofanyika Desemba 17.

Kabla ya uteuzi huu, mhandisi Nyamo-Hanga alikuwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA).

Mteule huyo pia ana uzoefu wa miaka 20 katika sekta ya nishati na pia amewahi kushika nyadhifa mbalimbali tangu mwaka 2008 alipoajiriwa Rea.

Wasifu wake
Mteule huyo ana Shahada ya uhandisi katika fani ya Umeme na Shahada ya Uzamili katika Menejimenti ya Uhandisi.

Pia, ana Shahada ya Uzamili ya Usimamizi wa Biashara (MBA) zote kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, akiwa pia na Stashahada ya Juu ya Sheria na Upatanishi na Usuluhishi ya Chuo cha Ustawi wa Jamii Dar es Salaam.

Rea inaomba sekta mbalimbali kumpatia ushirikiano mhandisi huyo ili kumuwezesha kutekeleza majukumu

Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Laptop City

Tangazo