Tamaa chanzo cha mimba za utotoni


Bahati Othmani, Hai

TAMAA ya kupata mali kwa baadhi ya makabila imeelezwa kuwa ni sababu kuu ya kuendelea kuongezeka kwa tatizo la mimba na ndoa za utotoni.

Suala hilo pia limeelezwa kuchangia watoto wa kike kukosa haki yao ya msingi ya kupata elimu.

Kauli hiyo imetolewa na washiriki wa mafunzo ya mradi wa majaribio wa kukabiliana na mimba na ndoa za utotoni unatekelezwa na shirika lisilo la kiserikali la Action For Justice in Society (AJISO) katika wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro

Kwa nyakati tofauti washiriki wa mafunzo hayo walieleza kuwa tatizo hilo bado ni sugu na zinahitajika jitihada za makusudi kulidhibiti kwa faida ya jamii.

Anna Samweli alisema kuwa tamaa ya fedha na mali imekuwa chazo kikuu cha watoto wa kike kupata mimba na ndoa za utoto kutokana na baadhi ya wazazi kuwalazimisha watoto hao kuolewa katika umri mdogo.

Mwenyekiti wa dawati la jinsia na watoto kutoka kituo cha polisi Bomang’ombe, Happynes Eliufoo alisema tatizo la mimba katika wilaya hiyo linaendelea kuongezeka kutokana na baadhi ya wazazi kushindwa kutoa ushirikiano pindi tatizo hilo linapotokea pamoja na kuficha wanaohusika na matukio hayo

Alisema kuwa kwa kutumia kamati za ulinzi na usalama wa mtoto kwa kila kijiji pamoja na jamii katika kupaza sauti kwa lengo la kutetea na kulinda haki za watoto wa kike , ni njia nyingine nzuri katika kukabiliana na vitendo hivyo mitaani.

“Ni vema wananchi wote kuunganisha nguvu katika kusaidia kamati hizo zinafanya kazi ipasavyo kwa kutoa taarifa na kuacha tabia ya kuwafungia ndani watoto wanapofanyiwa vitendo hivyo, huku wengine wakimalizana wenyewe bila kufikishwa katika vyombo vya sheria”alisema Elifoo.

Kwa upande wake mwezeshaji kutoka Asasi ya elimu mwangaza Tanzania inayojihusisha na masula ya ukatili dhidi ya watoto, Michael Reubeni aliwataka washiriki wote kulinda watoto wa kike kwani wanaofanya vitendo hivyo wako katika familia, majirani na hata wakati mwingine walimu ambao wamepewa dhamana ya kukaa na kuwalinda watoto.

Alifafanua kuwa ili mradi huo uweze kufanikiwa ni lazima viongozi wote kwa pamoja kutumia kauli mbiu ya mradi ya “Tokomeza ndoa na mimba za utotoni hali ambayo itasaidia kuondoa unyanyasaji huo utapungua kwa asilimia kubwa.

Ni wajibu wa kila mmoja kuona ana jukumu la kusaidia utekelezaji wa mpango huu katika maeneo yake kama walivyoahidi mawaziri na kwa umoja ni dhahiri vitendo hivi vitakomeshwa na kuwalinda watoto.

Msimamizi wa mradi huo kutoka AJISO, Tatu Mruthu alisema kuwa lengo la kuongeza uelewa na stadi juu ya masuala ya afya ya uzazi kwa vijana wa kike ili wajikinge na mimba za utotoni, UKIMWI na tabia hatarishi hatimaye wamalize masomo yao salama.

Mruthu alisema unatekelezwa katika kata mbili wilayani hapa ambazo utafiti ulionyesha kuwa tatizo la mimba na ndoa za utotoni bado ni tatizo kubwa ambapo kwa awamu ya kwanza utatekelezwa katika vijiji vya Sanya Stationi,Tindigani kata ya KIA na vijiji vya Chemka na Rundugai kata ya Masama Rundugai
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Laptop City

Tangazo