Wagonjwa 300 wapokewa Krismasi


Salha Mohamed

WAGONJWA 289 wamepelekwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Kitengo cha wagonjwa wa dharura na ajali, wakati wa Krismasi.

Idadi hiyo ni kwa siku tatu kuanzia siku hiyo hadi juzi.

Akizungumza jana na JAMBO LEO, Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano kwa Umma, Aminiel Aligaesha alisema wagonjwa hao walifikishwa kitengo hicho kuanzia saa 12 asubuhi.

“Wagonjwa waliofikishwa hapa walitoka jijini na mikoa jirani,” alisema Aligaesha.

Alisema kati ya wagonjwa hao, 70 walihusishwa na ajali za magari.
Zingine ni za pikipiki, kupigwa risasi, ajali za moto, kuvamiwa na vibaka na wengine kuanguka.
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Laptop City

Tangazo