Bei mpya ya umeme mwezi ujao



 Emeresiana Athanas

MAMLAKA ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (Ewura), inatarajia kutoa uamuzi wa maombi ya kupandisha gharama za umeme yaliyotolewa na Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), mwishoni mwa mwezi huu.

Hayo yalisemwa Dar es Salaam jana na Mkurugenzi Mkuu wa Ewura, Felix Ngamlagosi kuwa Mamlaka inaendelea kuyafanyia uchambuzi wa kina maombi hayo ili kuja na mapendekezo kabla ya Januari mosi.

"Matarajio yetu ni kwamba hadi mwishoni mwa mwezi huu, tutakuwa tumemaliza na kutangaza, na hivyo hadi Januari yatakuwa tayari yametolewa," alisema.

Alisema bado Mamlaka iko kwenye uchambuzi na baada ya kukamilisha uamuzi wa maombi hayo utatolewa.

Tanesco iliwasilisha maombi ya kupandisha gharama za umeme kwa asilimia 18, ambalo ni agizo la kubadilisha bei ya umeme la mwaka huu lililoanza Aprili mosi.

Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Laptop City

Tangazo