Sumatra yakaribisha mabasi ya muda


Edith Msuya

MAMLAKA ya Udhibiti wa Usafiri wa Majini na Nchikavu (Sumatra) imeanza kutoa vibali vya magari ya muda kwa ajili ya abiria watakaokwenda mikoani katika msimu wa siku kuu za mwisho wa mwaka.

Akizungumza jana Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Udhibiti wa Usafiri wa Barabara wa Sumatra, Johansen Kahatano alisema magari hayo yameandaliwa ili kujiandaa na ongezeko la abiria hasa msimu huu wa sikukuu.

Kahatano alisema matangazo yametolewa kuongeza magari hayo, ili kusaidia kwa kupambana na ongezeko la abiria kama likitokea katika kipindi hiki.

Alisema kwa sasa abiria si wengi kama ilivyokuwa awali, lakini magari hayo, ni msaada kama tatizo la magari litajitokeza na kusababisha abiria kupata shida.

"Japokuwa kwa sasa abiria si wengi, lakini kutokana na kukaribia kwa sikukuu hizi, tutakuwa tumeandaa mazingira mazuri kwa abiria," alisema.

Hata hivyo, Kahatano alitoa mwito kwa abiria kutoa taarifa watakapokutana na mawakala wasio waaminifu wanaopandisha nauli.

"Nitoe mwito kwa abiria atakayepandishiwa nauli, ni vema atoe taarifa kwenye mamlaka husika, ili hatua zinazostahili zichukuliwe," alisema.
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Laptop City

Tangazo