ACT-Walendo wapinga Morocco kuitawala Sahara Magharibi


Abraham Ntambara

Zitto Kabwe
CHAMA cha ACT Wazalendo kimeendelea kulaani ukoloni wa Morocco kwa taifa la Sahara Magharabi na kimepinga juhudi zozote zinazofanywa na Serikali za kufifisha msimamo wa nchi kwa visingizio vya diplomasia ya uchumi.

Taarifa iliyotumwa kwa vyombo vya habari jana Dar es Salaam na Katibu wa Kamati ya Mambo ya Nje ya Chama hicho John Mbozu ilisisitiza juu ya msimamo wa Tanzania kuhusu Uhuru wa Sahara Magharibi.

"Tunalaani ukoloni wa Morocco kwa taifa la Sahara Magharibi, tunapinga juhudi zozote za kufifisha msimamo wetu kwa visingizio vya diplomasia ya uchumi, ACT Wazalendo tuko Pamoja na Watu wa Sahara Magharibi dhidi ya ukoloni wa Morocco," alisema Mbuzi.

Mbozu alieleza msisitizo wa mafungamano kati ya Tanzania na Watu wa Sahara Magharibi.

Alisema uongozi wa ACT Wazalendo mapema mwakani, unatarajia kufanya ziara maalumu ya kutembelea maeneo yaliyokombolewa na kushikiliwa na Chama cha Polisario ili kujionea maendeleo ya harakati za ukombozi na kuziunga mkono.

Mbuzu alieleza kuwa viongozi wa chama ambao wanahudhuria Mkutano Mkuu wa Vyama vya Kijamaa unaoendelea jijini Berlin Ujerumani, walifanya mazungumzo ya kina na viongozi wa Chama cha Kijamaa cha Polisario kinachopigania Uhuru wa nchi ya Sahara Magharibi inayokaliwa kimabavu na Morocco.

Alikumbusha kwamba Sera ya mambo ya nje ya nchi yetu Tanzania tangu wakati wa Baba wa Taifa ni kusimama na wanyonge na kubainisha kuwa msingi huo bado ni muhimu.

Alisema kwa sababu hiyo, ACT-Wazalendo walipinga ujio wa Mfalme wa Morocco nchini kwa kuwa taifa hilo bado linaikalia ardhi ya watu wanyonge wa Sahara Magharibi.

Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Laptop City

Tangazo